Tetesi za Chama kuondoka, Simba yatuliza mashabiki

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Jun 2024
Tetesi za Chama kuondoka, Simba yatuliza mashabiki

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amewataka Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu wakati uongozi ukifanya maboresho ya kikosi

Ahmed amesema kipindi hiki ambacho maboresho makubwa yanafanyika, yapo majina ya wachezaji walioachwa yanaweza kuwashtua lakini ni katika 'kuimarisha nyumba'

Wiki iliyopita Simba ilitangaza kuachana na wachezaji watano wakiwemo Saido Ntibazonkiza na Luis Miquissone. Lakini kumekuwa na tetesi kuwa Simba huenda ikampa mkono wa kwaheri kiungo Clatous Chama ambaye mpaka sasa bado hajasaini mkataba mpya

"Naomba msishtuke Wanalunyasi kuona nyumba yenu inabomolewa ili ijengwe mpya na imara zaidi," aliandika Ahmed katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Simba imeendelea na michakato ya maboresho ya kikosi ambapo Ahmed amesema wiki hii watakamilisha hesabu za usajili tayari kwa kikosi kuelekea Pre-season wiki ijayo

Simba inakwenda kuweka kambi ya wiki tatu katika Mji wa Ismailia huko Misri

ADVERTISE HERE

More Stories

Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
23m ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
1h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
1h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
4h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
6h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
7h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
7h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
9h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
10h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
10h ago
READ MORE β†’