Mo arejea Bodi ya Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Jun 2024
Mo arejea Bodi ya Simba

Rais wa heshima klabu ya Simba, Bilionea Mohamed Dewji ametangaza kurejea kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba kufuatia ombi la Salim Abdallah 'Try Again' aliyejiuzulu nafasi hiyo jana Juni 11, 2024

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Dewji amesema lengo la kurejea ni kuweka mambo sawa baada ya klabu hiyo kuwa na mwenendo mbaya kwenye mashindano mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitatu tangu aondeke kwenye nafasi hiyo

Aidha Dewji amesema amemuomba Try Again aendelee kuwa mjumbe wa Bodi, ombi ambalo limekubaliwa, na hivi karibuni atatangaza Wajunbe wengine watakaounda Bodi hiyo ili kuisimamisha upya Simba

"Ninarejea nikiwa na nguvu na ari mpya mpaka Simba itakaporejea kwenye hali yake ya kawaida"

"Nongozwa zaidi na ushabiki wa Simba, siyo uwekezaji, wala ufadhili wala udhamini. Sitaiacha Simba leo wala kesho," alisema Mo

Dewji ametaja mambo sita ambayo anaamini yamepelekea Simba kupoteza nguvu yake huku akiahidi kuyafanyia kazi

  1. Umoja: Hakuna umoja ndani klabu na kumekuwa na mgawanyiko uliotokana na makundi ya uchaguzi.
  2. Timu yenye ushindani: Benchi la ufundi halikuwa zuri hivyo kushindwa kutengeneza timu yenye ushindani.
  3. Usajili: Wachezaji wengi waliosajiliwa, viwango vyao havikuwa bora.
  4. Ukuaji wa wanachama: Eneo la mashabiki na wapenzi limedumaa hasa kutokana na kukwama kwa mchakato wa mabadiliko (transformation).
  5. Kutokuwepo kwa mkakati wa ukuzaji na uendelezaji wa vijana
  6. Miundombinu iliyoko Bunju kutokidhi mahitaji. Mohamed ameahidi kutatua changamoto hizo kwa kushirikiana na wenzake huku akiwataka wanasimba wote kuwa kitu kimoja, kumpa ushirikiano, kuzika tofauti zao na kuepuka migogoro.
ADVERTISE HERE

More Stories

Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
21m ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
1h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
1h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
4h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
6h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
7h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
7h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
9h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
10h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
10h ago
READ MORE β†’