Dube akana mkataba Azam Fc, atinga TFF

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Apr 2024
Dube akana mkataba Azam Fc, atinga TFF

Mshambuliaji wa Azam FC aliyeaga klabuni hapo Prince Mpumelelo Dube amefungua malalamiko TFF akidai hakusaini mkataba mpya zaidi ya mkataba ambao unaisha mwishoni mwa msimu

Inadaiwa kuwa mshambuliaji huyo ameukana mkataba ambao Azam FC wanasema aliusaini na unaisha mwezi Juni 2026

Mshambuliaji huyo ametinga TFF na mkataba ambao anasema ni halali ambao unafikia ukomo wake mwisho mwa msimu huu yaani Juni 2024 

Mshambuliaji huyo amepeleka nyaraka mbalimbali pamoja na vielelezo vingine kuthibishisha kuwa mkataba wake halali unatamatika mwishoni mwa msimu huu

Hivi karibuni mchezaji huyo aliwaaga Azam kupitia akaunti yake ya Instagram huku akiwashukuru watu mbalimbali katika klabu hiyo kama viongozi wa timu, idara mbalimbali pamoja na mashabiki wa klabu hiyo

Klabu ya Azam ilijibu mapigo Kwa kusema mshambuliaji huyo bado ni mchezaji wao kwani anao mkataba mrefu mpaka 2026

Klabu hiyo imeenda mbali na kumwambia mchezaji huyo kuwa kama anataka kuondoka afuate utaratibu wa kuvunja mkataba na sio kuaga akiwa bado ni mali yao

Kwa kujibu wa klabu hiyo ni kwamba thamani ya kuvunja mkataba wa mchezaji huyo ni 700m hivyo afike mezani na atimize matakwa ya kifungu hicho ili wamuachie huru

Azam FC imekuwa ikimuandikia barua mshambuliaji huyo kila baada ya siku tatu ikimhitaji aripoti kazini kuendelea na majukumu yake.

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
5h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’