Timu ya Al Ahly inatarajiwa kuwasili nchini leo tayari kwa mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Simba utakaopigwa Ijumaa, March 29 katika uwanja wa benjamin Mkapa
Wakati wapinzani wao wakitua leo, Simba ilirejea kutoka Zanzibar jana baada ya kukamilisha kambi ya wiki moja
Kikosi cha kocha Abdelhak Benchikha kitakuwa na nafasi ya kujifua katika uwanja wa Benjamin Mkapa leo majira ya saa 3 usiku muda ambao mchezo dhidi ya Ahly utapigwa
Hii ni mechi muhimu sana kwa Simba kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali
Mchezo wa marudiano utapigwa April 04 huko Misri
ADVERTISE HERE