Matukio ya ushirikina yaiponza Simba TPLB

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Mar 2024
Matukio ya ushirikina yaiponza Simba TPLB

Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la mashabiki wake pamoja na walinzi wake wa uwanjani (stewards) kuhusika katika tukio la kuingia uwanjani na kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina wakati mchezo dhidi ya Mashujaa Fc ukiendelea kwenye uwanja wa Azam Complex Machi 15, 2024

Walinzi wa uwanjani (stewards) wa klabu ya Simba, Kessy Mohamed, Mrisho Mindu Pamoja na Mohamed Salmin pamoja na shabiki aliyefahamika kwa jina la Mohamed Saleh, wamefungiwa kuingia viwanjani kwa kipindi cha miezi 12 (kumi na miwili) kwa kosa la kushiriki katika tukio hilo

Aidha Bodi ya Ligi imeeleza kuendelea na uchunguzi wenye lengo la kufahamu wahusika wengine wa tukio hilo ambao hawakutambulika mara moja ili wachukuliwe hatua

Klabu ya Simba imetakiwa kuhakikisha mashabiki na viongozi walioadhibiwa wanatii adhabu zao na kuzitekeleza kikamilifu ili kuepuka adhabu zaidi

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
1h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
3h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
4h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
6h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’