Kocha Mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha amejipambanua kwa rekodi yake katika timu alizofundisha kabla ya kutua Msimbazi
Uwezo wake kimbinu umemfanya ajizolee sifa kwa kupata matokeo mazuri katika mechi za kimkakati
Wengi wanakumbuka kile alichofanya msimu uliopita wakati yuko ya USM Alger akiiwezesha timu hiyo kutwaa mataji mawili ya CAF yaani kombe la Shirikisho (CAF CC) na Super Cup akizifunga Yanga na Al Ahly
Ijumaa ya wiki hii Benchikha ataiongoza Simba katika mchezo mwingine ugenini ambao Simba haipaswi kupoteza
Mechi zake mbili alizocheza ugenini katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu aliweza kupata alama moja Botswana dhidi ya Jwaneng Galxy na kupoteza dakika za jioni dhidi ya Wydad Athletic lakini kikosi chake kikashinda mabao 2-0 katika mechi ya nyumbani
Benchikha amesema anatambua Asec Mimosas wana timu bora ndio maana wamekuwa timu ya kwanza kutinga robo fainali ya ligi ya mabingwa msimu huu hivyo wanakwenda kuchuana nao wakitambua ubora wao
"Tunakwenda kucheza na timu nzuri ambayo inacheza kitimu zaidi. Tuna malengo yetu tumeweka na lazima tutumie vyema kila nafasi tutakayotengeneza katika mchezo huo," alisema
Simba inahitaji ushindi au hata matokeo ya sare ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali
Mnyama atamaliza mechi ya mwisho hatua ya makundi nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy, hii ni mechi ambayo kisasi kitalipwa pale kwa Mkapa!