Simba yajipanga kusaka ushindi Ivory Coast

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Feb 2024
Simba yajipanga kusaka ushindi Ivory Coast

Baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kusogezwa mbele, Simba sasa inaelekeza nguvu zake katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Asec Mimosas ambao utapigwa Ijumaa, Februari 23 huko Ivory Coast

Huu ni mchezo muhimu sana kwa Simba ambayo inapiga hesabu za kutinga robo fainali ya michuano hiyo

Simba ikiwa na alama tano katika nafasi ya pili, inahitaji ushindi au hata alama moja tu ili kuwa katika nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali

Ni mechi ambayo Simba haipaswi kupoteza kwa gharama yoyote kwani matokeo hayo yatarejesha matumaini ya Wydad kusonga mbele

Wydad wana alama tatu ambapo kama watashinda mechi mbili zilizobaki watafikisha alama tisa

Simba itaweza kufikisha alama tisa kama itapata sare Ivory Coast na kushinda mechi ya mwisho nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy na inaweza kufikisha alama 11 kama itashinda mechi zote mbili zilizobaki

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
1h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
3h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
4h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
6h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’