Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika Yanga na Simba leo zimelazimishwa sare katika mechi za makundi ya michuano hiyo
Mchezo wa mapema kati ya Jwaneng Galaxy dhidi ya Simba uliopigwa Botswana ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Ulikuwa mchezo wa pili kwa Simba kulazimishwa sare katika michuano hiyo sasa ikifikisha alama mbili
Mchezo kati ya Yanga dhidi ya Al Ahly uliopigwa saa 1 usiku kunako uwanja wa Benjamin Mkapa, umemalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Pecy Tau alifunga bao la Al Ahly kwenye dakika ya 88 kabla ya Pacome Zouzoua kuisawazishia Yanga kwenye dakika za lala salama
Yanga inaendelea kubaki nafasi ya nne ikiwa na alama hiyo moja wakati Al Ahly ikiongoza kundi D ikiwa na alama nne
Nafasi ya pili CR Belouizdad yenye alama tatu sawa na Medeama Fc