Tetesi za soka Ulaya Jumanne, Novemba 28 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Nov 2023
Tetesi za soka Ulaya Jumanne, Novemba 28 2023

Manchester United wamemuuliza mshambuliaji wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Ujerumani Timo Werner na huenda wakamnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27mwezi Januari mwakani. (Sky Sports Germany)

Arsenal wanapanga kumnunua kiungo wa kati wa Aston Villa na Mbrazili Douglas Luiz, 25, Januari, huku mustakabali wa kiungo wa Ghana Thomas Partey, 30, The Gunners haujulikani. (ESPN)

Juventus wanatathmini uwezekano wa kumnunua Partey, na huenda wakasaidia kufadhili ofa ya Arsenal kumnunua Douglas Luiz. (Mirror)

Manchester City na Liverpool pia wanamtaka Luiz, 25, na wanatazamiwa kushindana na Arsenal kuwania saini yake. (90 min)

Chelsea wanapanga sera ya kusajili mchezaji mmoja ndani, mmoja nje ambayo inaweza kuwafanya wachezaji kadhaa kuondoka ili kutoa nafasi kwa wachezaji wapya. (Telegraph - usajili unahitajika)

Wachezaji wawili ambao wanaweza kuondoka The Blues ni beki wa Brazil Thiago Silva, 39, ambaye kandarasi yake inatamatika msimu ujao, na mlinzi wa Uingereza wa chini ya miaka-21 Trevoh Chalobah, 24, ambaye anauzwa. (Standard)

Manchester United wamemfanya mlinzi wa safu ya kati wa Crystal Palace wa Uingereza Marc Guehi, 23, kuwa lengo lao kuelekea uhamisho wa Januari. (Football Insider)

Manchester City na Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazovutiwa na mshambuliaji wa AC Milan wa Italia, Francesco Camarda, 15. (Tuttosport - usajili unahitajika, kwa Kiitaliano)

Tottenham na Arsenal ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka mshambuliaji wa Feyenoord wa Mexico, Santiago Gimenez, 22. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Wasaka vipaji wa klabu kadhaa za Ligi ya Premia wamekuwa wakifuatilia uchezaji wa mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood mwenye umri wa miaka 22 huko Getafe. (AS - kwa Kihispania)

Newcastle wanaweza kumnunua kwa mkopo mshambuliaji wa Paris St-Germain Mfaransa Hugo Ekitike, 21, mwezi Januari. (Caught offside)

Manchester City na Arsenal wametuma wasaka vipaji wao kumtazama kiungo wa FC Copenhagen raia wa Denmark, Tristan Aldcroft Panduro, 15. (Mail)

Winga wa Newcastle Muingereza Jacob Murphy, 28, ananyatiwa na Crystal Palace na Nottingham Forest kabla ya dirisha la usajili la Januari. (Football Insider)

Mmiliki wa Forest Evangelos Marinakis anazidi kufadhaishwa na kushindwa kwa klabu hiyo kuteua mtaalamu, jambo ambalo limesababisha shinikizo mpya kwa meneja Steve Cooper. (Telegraph - usajili unahitajika)

Bayern Munich wanavutiwa na mchezaji wa Barcelona Ronald Araujo, 24, lakini klabu hiyo ya Uhispania inataka kumbakisha beki huyo wa Uruguay. (Sky Sports Germany)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
1h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
1h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
2h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
3h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
4h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
6h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
8h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
9h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
10h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
11h ago
READ MORE β†’