Kocha wa Simba, Robertinho Oliveira amesema licha ya kikosi chake kuendelea kufunga mabao katika kila mechi, bado ipo changamoto kwenye safu ya ulinzi
Robertinho ameeleza kutofurahishwa na ukuta wake kuendeleza kuruhusu mabao jambo ambalo amesema hawapaswi kulifanya katika mechi zijazo ambazo ni ngumu
Aidha, Robertino amekiri kukosekana kwa Hennock Inonga ni changamoto kwani mara nyingi awapo uwanjani huwa ndiye kiongozi katika safu ya ulinzi
"Kwa muda mrefu tumekuwa tunamtumia Inonga (Henock), lakini sasa hayupo tunawatumia Che Malone na Kennedy. Wanafanya kazi kubwa, lakini tunatakiwa kuwaongezea kitu"
"Tunaweza kufunga mabao, lakini tunatakiwa kuongeza umakini na kuimarisha mawasiliano mazuri na mabeki wetu, ili wasiruhusu mabao katika mechi zijazo kwani zitakuwa ni mechi ngumu," alisema Robertinho
Robertinho amesema ataendelea kuboresha safu yake ya ulinzi na anaamini watakuwa tayari kwa mchezo wa Super Ligi dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa Oktoba 20 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa na marudiano kupigwa Oktoba 24 huko Misri