Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Oktoba 1 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Oct 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Oktoba 1 2023

Mshambuliaji wa Barcelona na Poland Robert Lewandowski, 35, amesalia kwenye orodha ya wachezaji ambao Saudi Pro League inataka kuwasajili. (Sport - kwa Kihispania)

Arsenal itaendelea kumfuatilia mshambuliaji wa Wolves na Ureno Pedro Neto kwa matumaini ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 katika uhamisho wa Januari. (Mirror)

Arsenal pia inamfuatilia mchezaji wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 19 na mlinzi wa Ivory Coast Ousmane Diomande. (Givemesport)

Mkurugenzi wa michezo wa Juventus Cristiano Giuntoli anasema Chelsea ilishindwa kumsajili mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 23 kwa sababu hawakutoa ofa ambayo ilikidhi thamani ya klabu hiyo ya Italia. (La Repubblica, kupitia Goal)

West Ham iliamua kutomsajili mshambuliaji wa Uingereza Jesse Lingard, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Nottingham Forest, kwa sababu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 hayuko sawa. (Football Insider)

Arsenal, Chelsea na Tottenham Hotspur wameonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Feyenoord na Mexico Santiago Gimenez, 22. (Fijaches - kwa Kihispania)

Shirikisho la soka la Saudi Arabia limewatafuta waamuzi wakuu wa Ligi Kuu ya Uingereza akiwemo Michael Oliver kuhusu kuchezesha Ligi ya Saudia. (Telegraph - usajili unahitajika)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Donyell Malen, 24, kutoka Borussia Dortmund huku akitafuta mchezaji wa kumsaidia winga wa Misri Mohamed Salah, 31. (Bild, via Express)

Bayern Munich wanajadiliana kuhusu uwezekano wa kumsajili tena beki wa zamani wa Ujerumani Jerome Boateng, 35, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Lyon mwishoni mwa msimu uliopita. (Sky Sports Ujerumani)

Everton wako tayari kumpa mlinzi wa England chini ya umri wa miaka 21, Jarrad Branthwaite, 21, mkataba mpya. (Football Insider)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
31m ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
1h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
4h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
6h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
7h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
7h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
9h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
22h ago
READ MORE β†’