Kikosi cha Simba kitaondoka nchini leo kuelekea Zambia tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania kufuzu hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Power dynamos
Mabasi mawili yaliyobeba mashabiki yaliondoka nchini jana kuelekea Zambia kuipa hamasa Simba katika mchezo huo ambao utapigwa Jumamosi, Septemba 16 katika uwanja wa Levy Mwanawasa
Jana Simba ilikamilisha maandalizi ya mwisho ikiwa na kikosi chake kamili isipokuwa kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza ambaye huenda akaungana na timu Zambia baada ya kuchelewa kwenye majukumu ya timu za Taifa
Simba inakwenda Zambia ikiwa na lengo moja tu, kushinda mchezo dhidi ya Power Dynamos ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga makundi
Simba imejiwekea malengo makubwa msimu huu, angalau kucheza nusu fainali ya michuano hiyo