Simba yafunguka kusajili makipa watano

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Sep 2023
Simba yafunguka kusajili makipa watano

Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba wamesema hawana shida yoyote kutokana na uamuzi wao wa kusajili idadi kubwa ya magolikipa kwa sababu imeandaa mikakati maalumu itakayohakikisha wachezaji hao wote wanatumika, imefahamika

Kwa sasa Wekundu wa Msimbazi ina makipa watano na idadi hiyo kubwa imetokana na mashindano mengi yanayowakabili, ikiamini wote watakaa langoni kuitumikia timu hiyo.

Makipa hao ni pamoja na Aishi Manula, Ally Salim, Hussein Abel, Ayoub Lakred na Ahmed Feruzi, aliyepandishwa kutoka katika timu ya vijana ya umri chini ya miaka 20 (U-20).

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema wamegundua moja kati ya sababu ambazo timu zote kubwa zinafanya vizuri kwenye michuano mbalimbali ya kimataifa ni kuwa na makipa wengi ambao ni bora na waliokamilika.

"Siyo dhambi kuwa na makipa wengi, tunataka tuwe na machaguo mengi, pia msimu huu tuna mashindano mengi kwa hiyo ni lazima tuwe nao wengi tena bora, niwakumbushe tu makipa tulionao si wale wa bora liende ni makipa kweli"

"Lakini tukaona twende Morocco kumchukua Ayoub Lakred, hii ni kuonyesha tumedhamiria kufanya vizuri na ukitaka kufanya vizuri ni lazima eneo la kipa lazima liwe zuri kwa asilimia 100, pia tuna kipa chipukizi, Ahmed Feruzi," alisema Ahmed.

Aliongeza usajili wa Lakred, raia wa Morocco ulitokana na Mbrazil, Luis Jefferson kuumia na Hussein alichukuliwa kwa ajili ya kuziba nafasi ya Beno Kakolanya.

"Hatujawasajili makipa wote hao kwa bahati mbaya kama watu wanavyodhani, kila aliyesajiliwa ilikuwa ni kwa sababu maalum na hakuna shida, ila tu kama hali itakwenda vinginevyo tunaweza kumtoa Feruzi, kipa wetu tuliyempandisha kutoka timu ya vijana chini ya miaka 20 kwa mkopo katika klabu nyingine ili aendelee kupata dakika nyingi za kucheza, ni kipa mzuri, tuna mipango naye ya muda mrefu, na kwa uwezo wake anaweza kuwa kipa namba moja katika timu yoyote ile ya Ligi Kuu hapa nchini," Ahmed alisema.

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
2h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
4h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
5h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
5h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
6h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
9h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
11h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
12h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
12h ago
READ MORE β†’