Tetesi za soka Ulaya, Jumatano August 16 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Aug 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatano August 16 2023

Manchester United ipo katika harakati za mwisho kutoa ofa rasmi kwa kiungo wa Fiorentina na Morocco Sofyan Amrabat, 26. (La Nazione - in Italian)

Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Alisson Becker hana mpango wa kuondoka Liverpool na ana furaha kuwa kipa namba moja wa meneja Jurgen Klopp. (Anfield Watch)

Timu ya Saudi Arabia Al-Nassr ilisemekana kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 na kwamba Alisson alikuwa na hamu ya kuhamia klabu hiyo. (Footmercato – In French)

Mshambulizi wa Misri Mohamed Salah, 31, ameripotiwa "kuitaka" timu ya Saudi Pro League kufanya mazungumzo na Liverpool kuhusu uwezekano wa uhamisho msimu huu. (Alkass, kupitia Football365)

Everton haijapokea ofa kutoka kwa Manchester United kwa kiungo wa Ubelgiji Amadou Onana, 21, na ni ada kubwa tu ya uhamisho itakayomzawadia kuondoka Goodison Park. (Liverpool Echo)

Manchester City wanatazamiwa kuwasilisha ombi jipya la kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na Brazil Lucas Paqueta, 25, katika saa 24 zijazo. (Football Insider)

Crystal Palace wanaamini kuwa Chelsea wamevuka mipaka katika mwenendo wao wakati wa kujaribu kumsajili winga wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Michael Olise, 21. (Mail)

Lazio imeanza mazungumzo na mlinda mlango wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris mwenye umri wa miaka 36 kuhusu uwezekano wa kuhamia Serie A ya Italia (Gianluca di Marzio - kwa Kiitaliano).

Fulham wamepokea ofa ya karibu pauni milioni 47 kutoka kwa Al-Hilal kwa mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akitaka kuhamia klabu hiyo ya Saudi Arabia. (TalkSport)

Liverpool wanafikiria kuwalenga wachezaji sita wa safu ya kati, akiwemo mchezaji wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 28, na kiungo wa kati wa Crystal Palace na Mali Cheick Doucoure, 23. (Mail)

Mkataba wa West Ham kumsajili beki wa Manchester United na England Harry Maguire umeporomoka kwa sababu wamechoka kumngoja mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kukubali kuondoka kwake Old Trafford. (Guardian)

Kuporomoka kwa mkataba huo kumepunguza uwezekano wa Manchester United kuweza kuweka makubaliano na Bayern Munich kwa beki wa Ufaransa Benjamin Pavard, 27. (Sky Sports)

Brighton wanavutiwa na beki wa kushoto wa Boca Juniors Valentin Barco huku Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 19 akisemekana kuwa na kipengele cha kumuachia cha takriban £8m. (Brighton Argus)

Kipa wa Uholanzi Tim Krul, 35, anatazamiwa kufanyiwa vipimo vya afya na Luton baada ya makubaliano kufikiwa na Norwich City. (Norwich Evening News)

Manchester City wameratibiwa kupokea 20% ya faida ambayo Southampton inapata kwa mauzo ya kiungo wa kati wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19, kwenda Chelsea. (Athletic)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
2h ago
READ MORE β†’
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
2h ago
READ MORE β†’
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
2h ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
3h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
5h ago
READ MORE β†’
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
17h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
19h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
19h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
20h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
21h ago
READ MORE β†’