Tetesi za soka Ulaya, Jumanne August 15 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Aug 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne August 15 2023

West Ham wanafikiria kujiondoa katika dili la mlinzi wa kati wa Manchester United Harry Maguire, 30, kwa sababu ya muda ambao inachukua kukamilisha. (Telegraph)

Iwapo uhamisho wa Maguire utatelekezwa bosi wa Wagonga nyundo hao David Moyes ataelekeza nia yake kwa mlinzi wa Ujerumani Jonathan Tah, 27, na mlinzi wa kati wa Ivory Coast Odilon Kossounou, 22, ambao wote wako Bayer Leverkusen. (Guardian)

West Ham wanataka kumbadilisha Mbrazil Lucas Paqueta, 25, katika kiungo na cha kati na mchezaji wa kimataifa wa Ghana na Ajax Mohammed Kudus, 23, ikiwa makubaliano yanaweza kufikiwa juu ya ada na Manchester City kwa mchezaji huyo wa zamani. (Talksport)

Brighton wako kwenye majadiliano juu ya mkataba wa pauni milioni 15 kumnunua kiungo wa kati wa Lille, Carlos Baleba, 19, wakiwa tayari wamekubaliana masuala ya kibinafsi huku wakitafuta kuziba pengo la Moises Caicedo kuelekea Chelsea. (Fabrizio Romano)

Liverpool, Newcastle United, AC Milan na Juventus ni miongoni mwa klabu ambazo zimekuwa zikimfuatilia Baleba. (Mail)

Beki wa Arsenal Gabriel ndiye mchezaji wa hivi punde zaidi anayelengwa kuhamia Saudi Pro League, ingawa The Gunners hawana shinikizo la kumuuza Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 25. (Mirror)

Tottenham wamemtambua fowadi wa Gent na Nigeria Gift Orban, 21, kama mchezaji atakayechukua nafasi ya Harry Kane baada ya kuhamia Bayern Munich. (Football Insider)

Nottingham Forest imeanzisha tena mpango wa kufanya kazi na George Syrianos, mkuu wa zamani wa uajiri wa klabu hiyo. (Subscription Required)

Aston Villa wanakaribia kukamilisha mkataba wa mkopo wa kiungo wa kati wa Italia Nicolo Zaniolo, 24, kutoka Galatasaray wakiwa na chaguo la kumnunua. (Sport Italia – In Itali)

Newcastle wamewasiliana upya na Arsenal kuhusu beki wa pembeni wa Scotland Kieran Tierney, 26, ingawa bei ya £30m ya The Gunners inaweza kuwa kikwazo. (Newcastle Chronicle)

Beki wa Chelsea Mhispania Marc Cucurella, 25, pia anamvutia mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe. (Telegraph – Subscription)

Manchester United, Bayern Munich, Real Madrid, Chelsea na Manchester City zote zilikataa nafasi ya kumsajili fowadi wa Paris St-Germain Neymar, 31, kabla ya Mbrazil huyo kujiunga na Al Hilal kwenye Ligi ya Saudia Pro League. (Independent)

Kujumuishwa tena kwa mshambuliaji Kylian Mbappe, 24, katika kikosi cha Paris St-Germain kunategemea mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo ya Ligue 1. (L'Equipe)

Everton wameanza mazungumzo na PSG kuhusu mkataba wa mkopo na chaguo la kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Hugo Ekitike, 21, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan na Eintracht Frankfurt. (RMC Sport – In French)

Jesse Lingard, 30, anaweza kujiunga tena na West Ham, na licha ya kufanya mazoezi na Inter Miami angependelea kucheza Ligi ya Premia. (Express)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
30m ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
1h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
4h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
6h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
7h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
7h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
9h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
22h ago
READ MORE β†’