Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa August 11 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Aug 2023
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa August 11 2023

Mshambuliaji wa England Harry Kane amefikia makubaliano na Bayern Munich kuondoka Tottenham na kujiunga nao kwa mkataba wa miaka minne. (Athletic)

Meneja wa Bayern Thomas Tuchel alimfanya Kane kuwa chaguo lake namba moja na atashangaa ikiwa nahodha huyo wa England hatajiunga na mabingwa hao wa Ujerumani. (Telegraph)

Tottenham watafikiria kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, ikiwa Kane atakwenda Bayern. (Gazzetta dello Sport)

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, amewarudia Paris St-Germain msisitizo wake kwamba hataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto kwa hali yoyote na anakusudia kumaliza kandarasi yake. (Le Parisien)

Liverpool sasa wanaongoza mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Brighton Moises Caicedo mbele ya Chelsea na wako tayari kuvunja rekodi ya ada ya uhamisho ya klabu hiyo ili kumnasa mchezaji huyo wa Ecuador mwenye umri wa miaka 21. (Sports)

Chelsea wanavutiwa na kiungo wa kati wa Italia Marco Verratti, 30, ambaye hayumo katika mipango ya meneja mpya wa PSG Luis Enrique. (Foot Mercato)

Inter Milan hawataki kufikia thamani Arsenal kwa Folarin Balogun na wamejiondoa kwenye mazungumzo kuhusu kumsajili mshambuliaji huyo wa Kimarekani mwenye umri wa miaka 22. (Calciomercato)

Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis anasema mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 24, atasalia na mabingwa hao wa Serie A kwa msimu ujao. (Sky Sports Italia)

Everton wameambiwa na Leeds kwamba mshambuliaji wa Kiitaliano Wilfried Gnonto, 19, hauzwi na sasa wako mbioni kumsajili mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 19 Youssef Chermiti kutoka Sporting Lisbon. (Liverpool Echo)

West Ham wanasubiri uamuzi kutoka kwa beki wa England Harry Maguire kuhusu kama atajiunga nao baada ya The Hammers kukubaliana ada ya £30m na Manchester United kwa ajjili ya mchezaji huyo mwenye miaka 30. (Mail)

Manchester City wameambiwa lazima walipe ada ya £80m ili kumsajili kiungo mshambuliaji wa Brazil Lucas Paqueta, 25, kutoka West Ham. (Teamtalk)

Real Madrid wanatamtaka mlinda mlango wa Hispania David de Gea, 32, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Manchester United, huku mlinda mlango wa Ubelgiji Thibaut Courtois, 31, akitarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na jeraha la goti. (Times)

Bayern Munich wametoa ofa ya kumsajili mlinda mlango wa Hispania Kepa Arrizabalaga, 28, kutoka Chelsea kwa mkopo na chaguo la kumnunua mwishoni mwa msimu. (Sky Sports)

Manchester City wanamfikiria mshambuliaji wa Stade Rennais na Ubelgiji Jeremy Doku, 21, kama mbadala wa winga wa Algeria Riyad Mahrez, 32, ambaye amejiunga na Al-Ahli. (Telegraph)

Burnley wamekubali mkataba wa pauni milioni 14 kumsaini kiungo mshambuliaji wa Uingereza Aaron Ramsey, 20, kutoka Aston Villa, ambaye wameweka kipengelea cha kumnunua tena kwenye mkataba huo. (Sports)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
29m ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
1h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
4h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
6h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
7h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
7h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
9h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
22h ago
READ MORE β†’