Robertinho asiingiliwe majukumu yake - Kibaden

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Aug 2023
Robertinho asiingiliwe majukumu yake - Kibaden

Mchezaji na kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni, amewataka wanachama na mashabiki wa Simba kuheshimu maamuzi ya Kocha Mkuu, Robertinho Oliveira, kutokana na kumtupia lawama kwa kutomchezesha straika Mzambia Patrick Phiri

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kibadeni anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao matatu 'hat-trick’' kwenye mechi ya watani wa jadi 'dabi' ya Simba na Yanga, alisema mashabiki wanamkosea kocha huyo kwani kitendo cha kumlazimisha kumchezesha ni kama vile wanamuingilia kwenye majukumu yake.

"Kitendo cha wanachama na mashabiki wa Simba kumshutumu kuwa hamchezeshi Phiri ni kama kumuingilia kwenye majukumu yake, yeye ndiye anayekaa na wachezaji na anawajua nani anatakiwa kucheza mechi hii na nani asubiri acheze lini, hii kulazimika kupangwa mchezaji kwa lazima si sawasawa kabisa," alisema Kibadeni

Mara baada ya Tamasha la Simba Day, ingawa alitambulishwa na kuonekana akipungia mashabiki kwenye orodha ya wachezaji 30, lakini hakucheza mechi hiyo, ikiwa ni mfululizo wa kutoonekana kwake uwanjani tangu msimu uliopita huku ikidaiwa kuwa ameshapona majeraha yaliyokuwa yanamkabili.

Kibadeni alisema hakuna kocha yeyote anayeweza kumuacha mchezaji mzuri nje au kupangiwa cha kufanya kwa sababu hata yeye anahitaji ushindi kuliko mtu yeyote na timu ikipoteza wao ndiyo hubeba lawama.

"Sisi makocha timu ikifungwa ndiyo tunabeba lawama kwa hiyo hakuna anayetaka kupoteza mechi kwa ajili ya kumuweka mchezaji mzuri nje, nadhani wawe wavumilivu tu kwa sababu anachokifanya na kukiona ni sahihi kwake kwa sasa na nadhani Simba ina mashindano mengi hakuna mchezaji atakayeweza kucheza mechi zote hizo. Najua atacheza tu wasiwe na haraka,"alisema Kibaden

Wanachama na mashabiki wa klabu hiyo licha ya kumshambulia kocha huyo kwenye mitandao ya kijamii, baadhi yao wamedai huenda kocha huyo anapata shinikizo kutoka kwa baadhi ya viongozi.

Mpaka sasa hakuna kiongozi yeyote wa Simba, wala Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally, aliyetaka kulizungumzia suala hilo ingawa kwenye akaunti yake yake ya instagram, baadhi ya mashabiki wamemwandikia kuwa kama kuna tatizo na mchezaji huyo walitatue haraka sana kwa sababu haileti taswira nzuri kwenye klabu.

Licha ya kukabiliwa na majeraha, msimu uliopita Phiri ndiye mchezaji aliyehusika kwenye mabao mengi zaidi katika klabu ya Simba

Alihusika katika mabao 22 kutoka mechi 26 alizoshiriki katika mashindano yote. Alifunga mabao 10 kwenye ligi kuu, mabao matano kwenye ligi ya mabingwa na mabao manne kwenye Ngao ya Jamii pia akitoa assist 3

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
2h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
4h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
5h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
6h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
6h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
9h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
11h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
12h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
12h ago
READ MORE β†’