Simba kuikabili Singida FG bila Chama

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Aug 2023
Simba kuikabili Singida FG bila Chama

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kutua mkoani leo kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Singida FG ambao utapigwa Alhamisi, August 10 katika uwanja wa Mkwakwani

Simba watacheza mchezo huo bila ya kiungo wao mshambuliaji Clatous Chama

Chama anatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting msimu uliopita

Chama alikosa mechi dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union katika msimu uliopita na mechi ya nusu fainali dhidi ya Singida FG itakuwa ya mwisho

Licha ya kumkosa Chama, kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira huenda asiwe na hofu yoyote kwani ana kikosi kipana chenye wachezaji bora zaidi ya mmoja katika kila nafasi

Luis Miquissone, Aubin Kramo, Willy Onana wote wanaweza kutumika katika nafasi ambayo hucheza Chama

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
9h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
11h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
12h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
13h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
13h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
16h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
18h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
19h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
19h ago
READ MORE β†’