Klabu ya Singida Fountain Gate imetangaza kuwa kambi ya maandalizi pre-season 2023/24 itafanyika mkoani Arusha
Singida Fountain Gate wametoa taarifa hii;
"Tunapenda kuwataarifu wadau na mashabiki wa Singida Fountain Gate FC kwamba maandalizi ya msimu ujao kwa klabu yetu yatafanyikia jijini Arusha kuanzia Julai 10, 2023.
Awali maandalizi yalikuwa yafanyikie kwenye nchi ya Tunisia lakini kutokana na ufinyu wa muda na kuchelewa kukamilika kwa zoezi la usajili wa wachezaji, tumelazimika kubaki nchini ili wachezaji wote waweze kushiriki maandalizi haya kwa wakati.
Taarifa zaidi kuhusu kambi yetu ya Arusha na maandalizi kwa ujumla zitaendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari na kurasa zetu za mitandao ya kijamii."
ADVERTISE HERE