Paris St-Germain wamemfanya mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 29, kuwa kipaumbele chao msimu huu baada ya kuondoka kwa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35. (Le Parisien - kwa Kifaransa)
Beki wa Uingereza Kyle Walker, 33, anataka kusalia Manchester City na yuko kwenye mazungumzo juu ya kuongezewa mkataba, licha ya Bayern Munich kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Mail)
Kiungo wa kati wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 28, amepokea ofa ya kujiunga na Saudi Pro League. (Athletic -Usajili unahitajika)
Mshambulizi wa Uingereza Marcus Rashford, 25, yuko mbioni kusaini mkataba mpya wa muda mrefu katika klabu ya Manchester United. (Mail)
Mshambuliaji wa Ujerumani Kai Havertz hana nia ya kusaini mkataba mpya Chelsea, huku mchezaji huyo wa miaka 24 akinyatiwa na Arsenal. (ESPN)
Arsenal imempa kiungo wa kati wa Ghana Thomas Partey, 30, ruhusa ya kutathmini uhamisho wa kwenda Saudi Pro League. (90 min)
Kipa wa Everton na England Jordan Pickford, 29, anaridhia kuwa Goodison Park na hajawasiliana na Manchester United. (Mail)
Napoli wana matumaini ya kufikia mkataba na mshambuliaji wao Victor Osimhen lakini wanakiri kwamba watazingatia ofa ya Mnigeria huyo mwenye umri wa miaka 24 msimu huu wa joto. (Metro)
Liverpool wanataka kumsajili kiungo wa Uholanzi Ryan Gravenberch, 21, kutoka Bayern Munich msimu huu wa joto. (Mirror)
Kiungo wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, 32, anasema wakala wake alitafutwa na Borussia Dortmund lakini ''hana mpango'' wa kurejea Bundesliga. (Goal)
Beki wa zamani wa Spurs na mchezaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland Matt Doherty, 31, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru, anahusishwa na Ligi ya Saudi Pro. (Sun)
Brighton wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Conor Gallagher, 23. (Football Insider)
BBC