Rais Samia abariki Tanzania kuandaa Afcon 2027

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 May 2023
Rais Samia abariki Tanzania kuandaa Afcon 2027

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Kenya na Uganda kupitia Pamoja Bid wamedhamiria kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwaka 2027 (AFCON 2027), imefahamika rasmi

Akizungumza jijini, Dodoma jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus, alisema nchi hizo zinawania nafasi hiyo kwa kutambua mafanikio makubwa ambayo sekta ya michezo imepata, hivyo kuwa wenyeji wa AFCON kutaongeza hamasa zaidi kwa ukuaji wa michezo hususan soka.

Alisema aidha michuano hiyo itachangia katika ukuaji wa utalii kwa kuwa ni mashindano ambayo hutazamwa na zaidi ya watu bilioni moja barani Afrika na maeneo mengine duniani kwa ujumla.

Vile vile, Rais Samia amesema mashindano hayo yataleta watu mashuhuri nchini wenye ushawishi duniani hivyo huwezesha na kunufaisha sekta nyingi za uchumi ambapo huchangia ajira, mapato kwa wafanyabiashara na serikali.

Kwa upande mwingine Rais Samia amesema Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeshafanya utafiti na kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji wa maandalizi ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Mashindano ya AFCON yataweka rekodi kwa mara ya kwanza kufanyika katika Ukanda wa Afrika Mashariki tangu yalipoanzishwa rasmi mwaka 1957.

Mwaka 2017, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri chini ya miaka 17 (AFCON U-17).

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
5h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
7h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
7h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
8h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
9h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
9h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
12h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
14h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
15h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
15h ago
READ MORE β†’