Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Ni matokeo ambayo yamepeleka huzuni kwa Ruvu Shooting kwani ni rasmi sasa Ruvu Shooting wameshuka daraja
Ruvu Shooting wana alama 20 huku zikiwa zimesalia mechi mbili ambazo hata wakishinda zote watafikisha alama 26
Mbeya City inayoshika nafasi ya 14 ina alama 27 ambazi haziwezi kufikiwa na Ruvu Shooting
Kwa upande wa Simba imepunguza gap la pointi dhidi ya watani zao Yanga baada ya kufikisha alama 67
Hata hivyo kama Yanga itapata ushindi katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji watatawazwa kuwa mabingwa wa Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo
ADVERTISE HERE