Santiago Bernabeu leo unapigwa mtanange wa nusu fainali ya mkondo wa kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid dhidi ya Manchester City
Timu mbili zenye safu bora za ushambuliaji barani Ulaya zitamenyana katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne huku Erling Haaland aliyevunja rekodi ya Manchester City akipambana na washambuliaji watatu wa Real Madrid Vinicius Jr, Rodrygo na Karim Benzema
Itakuwa ni mechi ya marudiano ya nusu fainali ya mwaka jana wakati Madrid ilipojizatiti na kufanikiwa kuwashinda City na kushinda taji la 14 lililoongeza rekodi
Lakini wakati huu wanakutana na Manchester City yenye Haaland aliyevunja rekodi za kupachika mabao huko Uingereza
Mnorwe huyo mwenye umri wa miaka 22 amefunga mabao 12 kati ya 26 ya City kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu
Anahitaji mabao matano zaidi kufikia rekodi ya Cristiano Ronaldo ya msimu mmoja ya mabao 17 akiwa na Madrid msimu wa 2013-14
Manchester City, inayoonekana kutozuilika kileleni mwa Premier League, inasaka kuwa timu ya pili ya Uingereza kushinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa, Ligi ya Premia na Kombe la FA baada ya wapinzani wao Manchester United kupata ushindi huo mwaka wa 1999
Real Madrid, inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa La Liga na ikiwa nyuma ya vinara Barcelona kwa pointi 14, watajipa moyo kwa kutwaa Kombe la Mfalme Jumamosi kwa mara ya kwanza tangu 2014
Na Madrid wana kawaida ya kuzifunga timu za Uingereza. Msimu huu wamezitupa nje Liverpool na Chelsea huku mwaka jana wakizifunga Chelsea, City na Liverpool na kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya