Nyota ya nahodha wa timu ya Taifa Tanzania na mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta imeendelea kung'ara baada ya juzi kufunga bao moja kwenye sare ya 2-2 dhidi ya Charleroi kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Ubelgiji
Samatta huu ni muendelezo wake wa kutupia mfululizo baada ya mchezo uliopita dhidi ya Anderlecht alifunga bao moja wakati timu yake (Genk) ikishinda 5-2
Nahodha huyu amefunga mabao sita kwenye kikosi cha Genk huku kinara wa mabao kwenye timu yao akiwa ni Paul Onuachu ambaye alifunga mabao 15 na ameondoka kwa sasa anakipiga Ligi ya Uingereza (Southampton)
Mabao ya Samatta kwenye mechi mbili mfululizo yamechangia Genk imalize ligi ikiwa na pointi 75 ikiwa kinara kwenye msimamo sawa na Union Saint-Gilloise na kwenda kwenye mchujo wa ubingwa huku ikiendelea kuongoza Ligi.
Genk kama ikifanikiwa kuchukua ubingwa basi itacheza Ligi ya Mabingwa kwa kuanzia hatua ya mchujo lakini kama ikimaliza nafasi ya pili basi itacheza kwenye raundi ya pili.