Talaka ya Hiba Abouk na Achraf Hakimi iliingia kwenye vichwa vya habari baada ya kuripotiwa kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 24 aliwasilisha malalamiko dhidi ya beki huyo wa pembeni wa Paris Saint-Germain
Mwanamke huyo alimshutumu Hakimi kwamba alidaiwa kumdhulumu kingono wakati mwigizaji huyo maarufu akiwa mbali na watoto wao
Gazeti la Kifaransa la First Mag liliripoti kwamba Hiba alikuwa akiomba nusu ya mali na utajiri wa Hakimi, lakini alishangaa alipojua kwamba hana chochote kwa jina lake
Mnufaika wa mshahara na mali ya Hakimi si mwingine ila mama yake, ambaye amekuwa akipokea ujira wake kwenye akaunti yake ya benki kwa miaka kadhaa.
Ijapokuwa habari hizo zimezua taharuki nchini Uhispania, Ufaransa na Morocco, imefahamika pia kwamba Abouk hayuko katika hali ambayo anahitaji sehemu ya utajiri wa aliyekuwa mume wake ili aweze kujikimu kimaisha, kwani ana utajiri mkubwa wa fedha. yake mwenyewe.