Simba yaipania Yanga dabi ya Kariakoo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Apr 2023
Simba yaipania Yanga dabi ya Kariakoo

Meneja wa habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wana kila sababu ya kupata ushindi siku ya Jumapili katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga ambao utapigwa April 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Ahmed alisema Simba imeingia rasmi katika wiki ya watani wa jadi ikiwa na dhamira ya kupata ushindi siku ya Jumapili

"Kwetu huu ni mchezo mkubwa sana. Lazima wachezaji wetu wajue wana kazi kubwa ya kuwarudishia furaha mashabiki wetu kwenye mechi hii ya Kariakoo Derby. Tunapata ushindi kwenye mechi ngumu zaidi, tutashindwaje kwa Yanga," alihoji Ahmed

"Sisi ndio wenyeji wa mchezo huo, tuna jukumu la moja kwa moja kutangaza mchezo huo, tunajukumu ya kutangaza maandalizi ya mchezo na timu"

"Kikosi kilirejea Dar jana usiku na leo kinaingia kambini. Jioni kitaanza mazoezi maalumu kuelekea kwenye mchezo, hali ya wachezaji ipo vizuri na hatuna majeruhi. Wachezaji waliopata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Ihefu tuliocheza Dar wote wapo vizuri"

"Mechi itakuwa Aprili 16, 2023 saa 11:00 jioni. Viingilio tayari vimetangazwa na TFF. Tiketi tayari zinapatikana vituoni na kupitia mitandao ya simu," alisema Ahmed

Akizungumzia utaratibu wa tiketi, Ahmed amesema kwa mara ya kwanza wametambulisha aina mpya ya tiketi ili kuwarahisishia mashabiki kukidhi mahitaji yao

"Kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya Kariakoo Dabi tutakuwa na tiketi za Executive. Tiketi itakuwa Tsh. 40,000 kwa mtu mmoja. Tutawapa gate pass na vinywaji wakiwa uwanjani. Tiketi zinauzwa kwa taasisi, mashirika au tawi na tiketi zinaanzia 20"

"Vile vile kwa mara ya kwanza tutakuwa na tiketi za Platinum. Tiketi moja ni Tsh. 150,000. Unapata usafiri kutoka na kurudi hotelini mkisindikizwa na polisi, chakula na vinywaji muda wa mapumziko pia kutakuwa na zawadi maalumu," alisema Ahmed

Simba pia imetambulisha Mnyama Tiketi ambapo kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Simba, Imani Kajula, amesema tiketi hizo ni maalum kwa mashabiki ambao wanapenda kwenda pamoja uwanjani

"Kuelekea mechi ya watani wa jadi, Simba inatangaza aina mpya ya tiketi ambayo ni Mnyama Ticket ambayo itawezesha marafiki ambao wanapenda kwenda pamoja uwanjani wanaweza kununua tiketi kama kundi"

"Hatupendi mashabiki wetu ambao wana kundi kupata shinda ya tiketi. Namba zitapatikana kwenye ofisi za Simba. Tunawaondolea changamoto ya kupanga foleni. Tunaamini siku ya Jumapili uwanja utajaa rangi nyekundu na nyeupe. Bei zinategemea na eneo," alisema Kajula

ADVERTISE HERE

More Stories

Arsenal yaandika historia Anfield, yaichapa Liverpool na kuimarisha uongozi kileleni
Arsenal yaandika historia Anfield, yaichapa Liverpool na kuimarisha uongozi kileleni
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yaiadhibu Kagera Sugar, yaibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0
Yanga yaiadhibu Kagera Sugar, yaibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0
4h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 4-0 Kagera Sugar, Ligi Kuu
Highlights : Yanga 4-0 Kagera Sugar, Ligi Kuu
4h ago
READ MORE β†’
Mnyama Simba SC yazindua jezi mpya kwa ajili ya CAF Champions League 2026/27
Mnyama Simba SC yazindua jezi mpya kwa ajili ya CAF Champions League 2026/27
5h ago
READ MORE β†’
TFF kusimamia uchaguzi wa Simba, ratiba kuboreshwa
TFF kusimamia uchaguzi wa Simba, ratiba kuboreshwa
9h ago
READ MORE β†’
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
12h ago
READ MORE β†’
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
12h ago
READ MORE β†’
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
12h ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
14h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
15h ago
READ MORE β†’