Akiwa bado hajasaini mkataba wa kuendelea kuitumikia PSG, kumekuwa na sintofahamu juu ya timu gani atacheza Lionel Messi msimu ujao
Messi (35) bado anatamani kushiriki soka la ushindani klabu nyingi zikijitokeza kumpa ofa nono ili ajiunge nazo
Kila kitu kinawezekana kuhusiana na wapi Messi atacheza msimu ujao, anasema mtaalam wa soka wa Uhispania Guillem Balague
Balague anasema nahodha huyo wa Argentina amepokea ofa kutoka Saudi Arabia na Ligi Kuu ya Marekani, huku kukiwa na nia ya kumrejesha Barcelona, ingawa bado hakuna ofa rasmi
Messi alikuwa amefikia makubaliano ya kimsingi ya kuongeza mkataba wake huko PSG kwa mwaka mwingine, na kipaumbele chake kuendelea katika kandanda ya Uropa hadi 2024
Baada ya misimu miwili huko Paris, klabu hiyo inayomilikiwa na Qatar Sports Investment, ingependa kumshawishi akubali mwaka huo wa ziada chini ya masharti aliyonayo sasa
Kulingana na Balague, Messi bado anahitaji kushawishika kuwa klabu hiyo ya Ligue 1 inaweza kubaki na ushindani katika kilele cha soka la Ulaya, huku mkurugenzi wa soka Luis Campos akitakiwa kupunguza mishahara ili kukidhi mahitaji ya Financial Fair Play.
"Messi alisema angekaa kwa mwaka huo wa ziada mradi tu kuwe na makubaliano ya pande zote mbili, ikiwa ni pamoja na kuhakikishiwa PSG itakuwa na ushindani zaidi ya ilivyo sasa" Balague alisema
"Ujumbe ambao Messi aliupata ni kwamba PSG itaweka sawa masuala yake ya kifedha, lakini wanapaswa kupunguza mishahara jambo ambalo linaifanya timu kukosa ushindani. Pia haijafahamika kama meneja atabadilishwa au la"
PSG wanaongoza Ligue 1 kwa pointi sita lakini jaribio lao la 11 mfululizo la kushinda Ligi ya Mabingwa lilimalizika kwa kushindwa kwa jumla ya mabao 3-0 na Bayern Munich katika hatua ya 16 bora mwezi uliopita.
Je, kweli Messi anaweza kurudi Barca? Messi aliondoka Barcelona kwa sababu za kifedha mnamo 2021 lakini timu hiyo imefanya jitihada kubwa kujiimarisha kiuchumi wakimuhakikishia Messi kurudi
Pamoja na kucheza Ufaransa, makazi ya Messi bado yako Mji wa Barcelona na pengine anaweza kushawishika kwenda kujiunga na waajiri wake hao wa zamani