Baada ya mapumziko ya takribani mwezi mmoja kupisha mechi za kalenda ya FIFA na CAF, ligi kuu ya NBC leo inaendelea katika mzunguuko wa 26 ambapo mechi mbili zinatarajiwa kupigwa
Walima alizeti wa Singida Big Stars watakuwa uwanja wa nyumbani, Liti kuikaribisha Polisi Tanzania
Ni mechi ambayo ina umuhimu wa kipekee kwa kila timu. Singida BS wanahitaji ushindi ili kuendelea kubaki nafasi ya tatu ambayo itawahakikishia kushiriki mashindano ya vlabu ya CAF msimu ujao wakati Polisi Tanzania wanahitaji ushindi ili kujinusuru na hatari ya kushuka daraja
Mchezo mwingine ni kati ya Azam Fc dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa dimba la Azam Complex, saa 3 usiku
Timu hizi zilikutana siku chache zilizopita kwenye mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na Azam Fc kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
Hii itakuwa mara ya tatu timu hizo zinakutana msimu huu Azam Fc wakishinda mechi mbili zilizopita
