Meneja wa Manchester United Erik ten Hag amethibitisha kuwa kiungo wa kati Christian Eriksen anakaribia kurejea kutoka kwa jeraha
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark amekuwa nje ya uwanja tangu Januari baada ya kuumia katika ushindi wa United wa Kombe la FA dhidi ya Reading Uwanja wa Old Trafford
Hapo awali Eriksen alitarajiwa kuwa nje hadi mwisho wa Aprili na labda hadi Mei, lakini kumekuwa na matumaini kuwa nyota huyo akarejea mapema zaidi
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 hayuko katika mpango wa United katika mchezo wa leo Jumatano dhidi ya klabu yake ya zamani Brentford lakini Ten Hag alikiri katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi kuwa Eriksen amerejea katika mazoezi kamili ya timu na ataongeza ubora unaohitajika katika eneo la kiungo
"Sio kwa kesho (leo) lakini anarudi uwanjani. Amerejea kwenye mazoezi ya timu kwa hivyo lazima tuone sasa jinsi anavyoweza kufanya maendeleo haraka, " alisema Ten Hag