Keita kuondoka Liverpool

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Apr 2023
Keita kuondoka Liverpool

Naby Keita ataondoka Liverpool msimu huu wa joto, na kuhitimisha kipindi cha miaka mitano huko Anfield. Mkataba wa kiungo huyo unamalizika Juni na atatafuta changamoto mpya nje ya Merseyside

Mchezaji mwenzake Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye pia atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu, pia anajiandaa kuondoka majira ya kiangazi.

Mwanahabari Fabrizio Romano alikuwa wa kwanza kufichua habari hizo, akichapisha kwenye mitandao ya kijamii

"Naby Keita ataondoka Liverpool kwa uhamisho wa bure. Hakuna mabadiliko kwenye mpango wake na Oxlade-Chamberlain, maamuzi yalifanyika tangu Novemba  na ndivyo itakavyokuwa kwa mkopo wa Arthur Melo."

 Keita aliigharimu Liverpool pauni milioni 52.75 kutoka kwa RB Leipzig mwaka 2018, lakini hakufikia matarajio.

Amecheza mara 129 na kufunga mabao 11 kwa wababe hao wa Premier League. Muda wake Anfield umekumbwa na matatizo ya majeraha na amekosa takriban mechi 84 kutokana na jeraha. Huku zikiwa zimesalia mechi 11 tu za msimu wao kumalizika, huenda akawa amecheza dakika zake za mwisho kwenye kikosi cha Jurgen Klopp

ADVERTISE HERE

More Stories

Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
22m ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
1h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
1h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
4h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
6h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
7h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
7h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
9h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
10h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
10h ago
READ MORE β†’