Klopp akiri mambo magumu Liverpool

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Mar 2023
Klopp akiri mambo magumu Liverpool

Mkufunzi wa Livepool Jurgen Klopp anasema wanakabiliwa na kazi kubwa kurejea katika Ligi ya Mabingwa baada ya kipigo cha Real Madrid

Majogoo hao walibomolewa 5-2 dimba la Anfield wiki tatu zilizopita na bao la dakika za lala salama la Karim Benzema kwenye Uwanja wa Bernabeu likafanya kushindwa kwa Liverpool kwa jumla ya mabao 6-2

Dalili sio nzuri kwa upande wao kwani wanahatari ya kutoshiriki ligi ya mabingwa msimu ujao kama fomu yao haitaimarika. Wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Premia alama sita nyuma ya Tottenham inayoshika nafasi ya nne

"Tulijiandaa kupambana lakini hatukuweza kupata matokeo tuliyoyahitaji uwanjani. Ilikuwa dhahiri, mpango wetu uliharibika tangu mchezo wa kwanza" alisema Klopp.

Nyota watatu ambao walikuwa na mchango mkubwa kuipeleka Liverpool kwenye fainali tatu za Ligi ya Mabingwa ndani ya miaka mitano, Sadio Mane aliondoka kwenda Bayern Munich msimu uliopita wa joto, Roberto Firmino anaondoka mwishoni mwa msimu huu huku Mohamed Salah akishindwa kufikia ubora ambao wengi walimuona katika misimu iliyopita

Nahodha Jordan Henderson anatimiza miaka 33 mwishoni mwa msimu na James Milner, aliyeanza Bernabeu, ana miaka 37

Kiungo wa zamani wa Scotland, Charlie Adam, ambaye aliichezea Liverpool 2011-12, alisema Klopp anahitaji kukiongezea nguvu kikosi chake

"Nadhani Jurgen Klopp amekuwa mwaminifu sana kwa wachezaji hawa, lakini nadhani anahitaji nguvu mpya kwenye kikosi chake"

ADVERTISE HERE

More Stories

Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
21m ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
1h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
1h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
4h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
6h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
7h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
7h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
9h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
10h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
10h ago
READ MORE β†’