Mabao mawili aliyofunga kwenye mchezo dhidi ya Pan African uliopigwa uwanja wa Highland Estate Mbarali jana, yamemfanya mshambuliaji wa Ihefu Fc Andrew Simchimba aongoze mbio za wafungaji bora kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Simchimba amefikisha mabao saba akimuondoa kileleni mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize mwenye mabao sita
Mzize nae alifunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons hivyo kufikisha mabao sita
Mshambuliaji wa Simba Moses Phiri ni miongoni mwa wachezaji waliofunga mabao mengi kwenye michuano hiyo akiwa na mabao manne
Ushindi wa mabao 2-0 ambao Ihefu Fc waliupata dhidi ya Pan African uliwahakikishia kutinga robo fainali wakiungana na Simba, Yanga, Singida BS, Mtibwa Sugar na Geita Gold
Mechi mbili za kukamilisha timu nane hatua ya robo fainali zinapigwa leo Kagera Sugar ikiumana na Mbeya City wakati Azam Fc ikichuana na Mapinduzi Fc