Msafara wa kikosi cha Simba utaondoka nchini leo Alhamisi jioni kuelekea Uganda kwa ajili ya mchezo wa ligi ya Mabingwa dhidi ya Vipers Fc
Mchezo huo utapigwa Jumamosi jioni, Februari 25 2023
Msafara wa Simba utajumuisha wachezaji 25, benchi la ufundi na baadhi ya viongozi
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Simba mapema, kikosi kitakamilisha mazoezi ya mwisho kabla ya kuanza safari
Baada ya kupoteza mechi mbili za mwanzo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, Simba ina kibarua cha kusaka alama tatu ugenini ili kufufa matumaini ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo
ADVERTISE HERE