Msuva apania kuibakisha Al-Qadsiah daraja la Kwanza

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Feb 2023
Msuva apania kuibakisha Al-Qadsiah daraja la Kwanza

Mshambuliaji Mtanzania anayeitumikia Al-Qadsiah, Simon Msuva anapambana kuhakikisha anaikwamua timu hiyo isishuke daraja, kutokana na nafasi ya 15 iliopo sasa, huku ikiwa imebakiza mechi tatu tu kufunga msimu

Katika mechi 21 iliyocheza timu hiyo, imeshinda tano, sare saba, imepoteza tisa na imevuna pointi 22, ina jumla ya mabao 15, huku Msuva akifunga saba katika mechi saba sawa na kusema kuwa amefunga nusu ya mabao yote.

Ili Al-Qadsiah isishuke daraja inatakiwa ishinde mechi tatu zilizobakia, kwani timu tatu zilizopo chini yake ambazo ni Al Sahel ina pointi 20, Najran ina pointi 18 na Shoulla pointi 11.

Msuva amesema anajiona ana kazi nzito ya kuitetea timu yake, hivyo anahitaji kufunga mabao mengi zaidi na ikiwezekana amalize na mabao 15 ambayo yatakuwa yakiipa ushindi wa kupata pointi timu hiyo.

"Timu yangu haipo nafasi nzuri, hivyo naelekeza nguvu zangu, akili zangu zote nazipeleka hapa kuhakikisha nafunga mabao ya kupata pointi kwa maana timu ishinde na siyo sare ama kufungwa hiyo ndio itakuwa furaha yangu," alisema Msuva

ADVERTISE HERE

More Stories

Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
1h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
1h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
2h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
3h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
4h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
6h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
8h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
9h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
10h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
11h ago
READ MORE β†’