Tottenham ni miongoni mwa timu zinazovutiwa na kiungo wa kati wa Leicester City na Uingereza James Maddison, 26. (Mirror)
Spurs hawatamruhusu fowadi wa Uingereza Harry Kane, 29, kujiunga na mpinzani wa Premier League msimu huu - bila kujali bei - huku klabu za Manchester United na Bayern Munich zikimnyatia. (90 min)
Mshambulizi wa kimataifa wa Marekani Christian Pulisic, 24, ni miongoni mwa wachezaji ambao huenda wakauzwa na Chelsea Pamoja na wing awa Morocco Hakim Ziyech, 29, na mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29 - ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Inter Milan. (ESPN)
AC Milan wanatazamia kufufua nia yao ya kumnunua mshambuliaji wa Arsenal na England chini ya umri wa miaka 21 Folarin Balogun, 21, ambaye kwa sasa anang'ara kama mfungaji bora wa Ligue 1 akiwa kwa mkopo Reims. (mail)
Milan pia wanamtaka kiungo wa kati wa Liverpool na Guinea Naby Keita, 27. (Mirror)
Liverpool na Newcastle wamefanya mazungumzo kuhusu uwezekano wa kumnunua beki wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Jonathan Tah, 26. (90min).
Manchester United iko tayari kumsajili kiungo wa Austria Marcel Sabitzer, 28, kwa mkataba wa kudumu msimu wa joto ikiwa atavutia wakati wa kipindi chake cha mkopo kutoka Bayern Munich huko Old Trafford. (ESPN)
Tottenham huenda ikamnunua kinda wa Benfica, Rui Pedro Braz iwapo mkurugenzi wao mkuu wa soka Fabio Paratici atafungiwa duniani kote baada ya kuhusishwa na kashfa ya kifedha inayoikumba Juventus. (Mirror)
Mshambulizi wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 33, atasusia kuhamia Los Angeles FC na kupigania nafasi yake Chelsea. (Telegraph -subscription Rrequired)
Manchester United, Arsenal na Liverpool zote zimefanya mazungumzo na wakala wa mshambuliaji wa Barcelona na Uhispania Ansu Fati, 20. (Fabrizio Romano)
Manchester United pia inamfuatilia kiungo wa kati wa Royal Antwerp na Ubelgiji Arthur Vermeeren mwenye umri wa miaka 18. (Mail)
Mshambulizi wa zamani wa Leeds United Jimmy Floyd Hasselbaink anaamini kuwa klabu hiyo ya Elland Road inafaa kumtazama Steven Gerrard katika kutafuta meneja mpya. (Casinos En Ligne, via Yorkshire Evening Post);
BBC