Baada ya kurejea kutoka nchini Misri kikosi cha Simba kimepewa mapumziko ya siku nne hadi Jumamosi kuendelea na maandalizi ya michezo ya ligi kuu ya Vodacom.
Simba iliondoshwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika na Al Masry licha ya kutoka suluhu ya bila kufungana Jumamosi iliyopita.
Matokeo ya mabao 2-2 iliyopata Al Masry kwenye mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa March 07 ndiyo yaliyoiondosha Simba kwenye mashindano.
Wakati wachezaji wengine wakipata mapumziko, Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na Shiza Kichuya wao wameungana na kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kinachosafiri nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kirafiki keshokutwa, March 22, 2018.

ADVERTISE HERE