FT : Simba 1-1 Mtibwa Sugar

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Oct 2017
FT : Simba 1-1 Mtibwa Sugar
Emanuel Okwi aliifungia Simba bao muhimu la kusawazisha kwenye dakika za majeruhi na kuiwezesha timu yake kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mtibwa Sugar ndio iliyoanza kutikisa nyavu za Simba mapema katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Stamili Mbonde aliyeunganisha wavuni mpira wa kona.

Simba ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi lakini ilikosa mbinu ya kuipenya ngome ngumu ya Mtibwa Sugar ambayo ilitumia mbinu ya kujihami.

Hata hivyo wakati mchezo huo ukielekea ukingoni Okwi alifanyiwa majeruhi nje kidogo ya boksi la 18 ambapo yeye mwenyewe akachukua majukumu ya kuujaza mpira huo wavuni.

Aidha katika mchezo huo Simba ilipata pigo la kuwapoteza wachezaji wake Salim Mbonde na John Bocco walioumia na nafasi zao kuchukuliwa na Juuko Murshidi na Juma Luizio.

Matokeo hayo yameirudisha Simba kileleni kwa tofauti ya mabao baada ya kufikisha alama 12 sawa na Mtibwa Sugar, Yanga na Azam FC.

Kwenye mchezo mwingine, Tanzania Prisons imelazimishwa suluhu ya bila kufungana na Stand United.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’