Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina anatarajiwa kuwasili leo jijini Dar es salaam akitokea kwao Zambia alikokuwa mapumziko.
Taarifa za awali zilibainisha kuwa Lwandamina ilikuwa awasili jana na klabu ya Yanga ingeanza maandalizi ya msimu mpya kesho Julai 04.
Lwandamina alipitia Swaziland kumshuhudia mmoja wa viungo wanaowaniwa na Yanga Kabamba Tshishimbi.

Tshishimbi anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji klabu ya Mbabane Swallows amependekezwa na kocha Lwandamina mwenyewe.
Tshishimbi jana alikuwa kwenye kikosi cha Mbabane kilichokuwa kinachuana na CS Sfaxien ya Tunisia katika mchezo wa hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alionekana kwa mara ya kwanza wakati Mbabane ilipokuja jijini Dar es salaam kuchuana na Azam FC katika mchezo wa kwanza, hatua ya mtoano kombe la shirikisho.
Lwandamina amedhamiria kuimarisha sehemu ya kiungo na hakika kama Tshishimbi na Zamiselemi Moyo wote watapatikana basi wapinzani waandike maumivu.
Baada ya kuwasili kwa Lwandamina huenda Yanga ikaweka hadharani majina ya wachezaji walioachwa pia kutangaza wachezaji waliosajiliwa(ambao uhamisho umekamilika).
Dirisha la usajili la VPL lilifunguliwa Juni 15 na linatarajiwa kufungwa Agosti 06.

ADVERTISE HERE