Simba kuweka kambi ya muda Cairo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Mar 2018
Simba kuweka kambi ya muda Cairo
Wekundu wa Msimbazi, Simba wataondoka nchini keshokutwa Jumatano kuelekea Cairo, Misri ambapo wataweka kambi ya muda kabla ya kuwafuata wenyeji wao, Al Masry.

Al Masry inatarajia kuikaribisha Simba Jumamosi katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Machi 7 kwenye Uwanja wa Taifa jijini.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kikosi cha timu hiyo kitaondoka nchini keshokutwa na kitaweka kambi ya muda jijini Cairo na siku inayofuata itaanza safari kuelekea Port Said.

Manara amesema kuwa maandalizi ya safari yameshakamilika na kinachosubiriwa ni Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre, kutoa orodha ya mwisho ya wachezaji watakaosafiri.

"Idadi ya wachezaji itaamuliwa na kocha, yeye ndiye anayejua askari ambao watamfaa kwenye vita hii tunayokwenda kuikabili, kwa upande wa viongozi, kila kitu kinakwenda vyema, sisi ndio wazoefu wa mashindano ya kimataifa," alisema Manara.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’