Kesho Jumamosi Novemba 25 Yanga inashuka kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi kucheza mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 11 dhidi ya Prisons.
Mchezo huo ulihamishiwa kwenye uwanja wa Azam baada kutolewa kwa taarifa na Serikali kuwa uwanja wa Uhuru utakuwa na matumizi maalum kesho.
Yanga itaingia Chamazi ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mbeya City wiki iliyopita.
Prisons ni moja ya timu ambazo hazifungiki kwa urahisi msimu huu. Lakini Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikihitaji ushindi zaidi ili kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi.
Kikosi cha Yanga kitakachokabiliana na Prisons kinaweza kisiwe na mabadiliko makubwa ukilinganisha na kikosi kilichopata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mbeya City.
Badiliko pekee linalotarajiwa ni pengine kujumuishwa kikosini kwa mshambuliaji Amissi Tambwe ambaye huenda akapata dakika kadhaa kwenye mchezo huo baada ya kurejea dimbani ikiwa ni miezi minne tangu aumie goti.
Viungo Papi Tshishimbi na Thabani Kamusoko huenda wakakosekana kwenye mchezo huo kwa kuwa bado hawako fiti.
Hata hivyo kiungo Pato Ngonyani amekuwa akifanya vizuri tangu aaminiwe na kocha George Lwandamina huku Raphael Daudi Lothi, kiungo mshambuliaji sasa akiwa kwenye kiwango bora zaidi ndani ya kikosi cha Yanga.
Yanga ina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi mnono kwenye mchezo huo.

ADVERTISE HERE