Wakati homa ya pambano la watani wa jadi ikizidi kupanda, mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni ameitabiria Simba ushindi, lakini ametahadharisha kuwa hautakuwa mchezaji mwepesi
Kibaden amesema hana mashaka na ubora wa Simba lakini hawapaswi kuwadharau wapinzani wao Yanga
"Ukilinganisha timu hizi mbili ndani ya uwanja, utaona Simba ni bora kuliko Yanga, lakini benchi la ufundi na wachezaji wa Simba hawapaswi kukaa vichwani mwao ni vyema wakaingia uwanjani wakihisi wanacheza na timu ngumu ," alisema

Kibadeni anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao matatu 'hat-trick' kwenye mechi moja ya watani wa jadi, alisema siku zote mchezo unaozikutanisha timu hizo mbili unakuwa na vitu vingi vya ndani na nje ya uwanja, hivyo ni vyema wachezaji wakaweka nguvu zaidi kupambana uwanjani
Alisema amezifuatilia timu hizo katika mechi kadhaa msimu huu na ameona Simba wana nafasi kubwa ya kupata ushindi endapo watacheza kwa kujitoa kama walivyokuwa wakifanya kwenye mechi za kimataifa