Subirini mziki wa Tuisila

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2020
Subirini mziki wa Tuisila

Aliyewahi kuwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera, ameipongeza klabu hiyo kwa kufanikiwa kumnasa winga machachari kutoka AS Vita Tuisila Kisinda

Zahera ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu ya Gwambina Fc iliyopanda daraja msimu huu, amesema ujio wa nyota huyo kwenye kikosi cha Yanga utawapa faida nyingi

Zahera amesema kwa maoni yake, kuondoka kwa winga Bernard Morrison na kujiunga na Simba hakuwezi kuwa tatizo tena kwa Yanga kwani wamesajili mchezaji bora zaidi

"Huyu Tuisila ni mchezaji mzuri sana, ni zaidi ya Morrison. Huyu ni mchezaji anayeweza kufanya kazi zaidi ya moja uwanjani, anafunga, anapiga chenga lakini pia ni mzuri sana kwenye mipira ya vichwa"

"Nadhani ni moja ya sajili bora ambayo Yanga imefanya mpaka sasa,"alisema Zahera

Usajili wa Tuisila umekuwa saprise kwa wengi kwani kinda huyu alikuwa mmoja wa wachezaji wa kutegemewa katika kikosi cha kwanza cha AS Vita

Anakuja Yanga kuendeleza moto aliokuwa nao kule AS Vita

Simba watakuwa wakimkumbuka vizuri mwamba huyu kwani katika kile kipigo cha mabao 5-0, walichofungwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa mwaka juzi, Tuisila alikuwa mmoja wa wafungaji wa mabao ya AS Vita lakini pia alitengeneza bao moja pia akichaguliwa kuwa nyota wa mchezo ule

Kisinda na kiungo Mukoko Tonombe wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam kesho Alhamisi, saa saba mchana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’