Rasmi, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia atatetea kiti chake kwa miaka mingine minne
Ni baada ya kutangazwa kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Urais baada ya wagombea wengine wawili Hawa Mniga na Evance Mgeusa kukosa sifa za kuendelea na uchaguzi kwa hatua inayofuata.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Benjamin Kalume amesema, Karia anasubiri kuthibitishwa na Mkutano Mkuu lakini si kupigiwa kura tena
ADVERTISE HERE