Jumamosi ijayo, August 22 2020 Yanga itazindua rasmi wiki ya Mwananchi kule mkoani Dodoma, Makao Makuu ya nchi
Hili litakuwa tukio la kwanza kubwa kabla ya tukio la pili la kuhitimisha wiki hiyo ambalo litafanyika jijini Dar es salaam kwa mchezo wa kukata na shoka ambao utapigwa uwanja wa Taifa wa Mkapa
Mchezo huo ndio utatumika kukitambulisha kikosi cha Yanga tayari kwa msimu mpya
Kabla ya Jumamosi, mambo mengi yatatokea hapa katikati. Injinia Hersi yuko anga za mbali akikamilisha michakato ya usajili wa nyota wa kigeni ambapo baadhi inaelezwa watatambulishwa kule mkoani Dodoma
Kuhusu kocha mkuu, taarifa za uhakika ni kuwa Yanga imeshampata, kinachosubiriwa kwa sasa ni kukamilika kwa taratibu za kiofisi kabla ya kumtambulisha pamoja na benchi lake la ufundi
Lakini pia linakuja tukio jingine kubwa la uzinduzi wa jezi. Mashabiki wanasubiri jezi hizo kwa shauku kubwa ili waweze kuchangia juhudi zinazoendelea
Simba walizindua jezi wiki iliyopita, jezi zao zimekosa mvuto wa kibishara, sasa kinasubiriwa kishindo cha GSM
Uzi wa msimu uliopita bado unafanya vizuri sokoni lakini huo uzi mpya ni funga kazi...!