Simba imerejea jijini Dar es salaam jana wakitokea Ruvuma ambako walifanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa kuichapa Azam Fc bao 1-0
Mabingwa wa nchi wamerejea kujiandaa na mchezo dhidi ya watani zao Yanga utakaopigwa mwishoni mwa wiki
Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema anaamini vijana wake, wamefanya kazi nzuri Songea na bila shaka watashinda mataji yote mawili yaliyobaki
"Nakiamini sana kikosi changu, Simba ni moja ya timu ambayo ina kikosi bora zaidi msimu huu, tulijua tutapata ushindani mkubwa kutoka kwa Azam lakini tulikuwa tumejipanga kushinda"
"Kama nilivyosema huko nyuma malengo yetu msimu huu ni kuchukua mataji yote ya ndani na tunakaribia kuchukua ligi na tumeingia fainali FA ngoja tuone itakuwaje huko mbele," amesema Gomes
Simba imepania kutangaza ubingwa mapema Julai 03 dhidi ya watani zao katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa