Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano klabu ya Yanga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said, amesema yuko DR Congo kukamilisha usajili wa wachezaji kutoka AS Vita na sio kocha
Jana Baada ya kutua DR Congo, Hersi alipokewa na Makamu Mwenyekiti wa AS Vita pamoja na kocha Florente Ibenge na hivyo kuibua sintofahamu miongoni mwa mashabiki wa Yanga kwani inafahamika mabingwa hao wa kihistoria bado hawajamtangaza kocha wao mkuu
"Kilichonileta hapa Congo ni kukamilisha usajili wa wachezaji tuliowahitaji, sio kocha. Ibenge ataendelea kuwa kocha wa AS Vita," alisema Hersi
Aidha, Hersi amesema lengo lao kuunda timu imara ndio maana wanasajili wachezaji ambao wanaamini watawasaidi bila ya kujali wamemaliza mikataba au la
"Klabu ya Yanga inafanya biashara ya Mpira ambayo ni halali na inanunua wachezaji wenye mikataba na walio bora na ndio maana wengi tunaowaleta tumevunja mikata yao kwenye vilabu vyao na wenye umri mdogo na sio wazee," aliongeza Hersi
Kuna nyota wawili kutoka klabu ya AS Vita wanatarajiwa kutua Yanga baada ya kukamilishwa kwa usajili wao
Huu ni ujumbe tosha kwa wale waliokuwa wakibeza usajili wa Yanga, kwani GSM wamesimamia kwenye ahadi yao kuwa watasajili wachezaji wote waliohitajika