Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amewapongeza wachezaji kwa kiwango bora na kuendelea kuibuka na ushindi mfululizo katika ya ligi kuu ya Vodacom
Jana Simba iliifumua Mbeya City mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Ni ushindi ulioisogeza Simba karibu na ubingwa sasa wakihitaji alama tatu tu kutangaza ubingwa
Akizungumza baada ya mchezo jana, Gomes alisema sasa wanahitaji kumaliza kazi kwenye mchezo ujao dhidi ya Yanga
Gomes raia wa Ufaransa, amesema mchezo dhidi ya Yanga utakuwa kama fainali kutokana na umuhimu wa matokeo yake
"Nawapongeza wachezaji wangu, tunacheza vizuri, tunashinda mechi nyingi mfululizo na naamini itakuwa hivyo hadi mwisho wa msimu"
"Tumebakisha mechi tano na tunahitaji alama tatu tutangazwe mabingwa na mchezo unaofuata ni dhidi ya watani wetu Yanga najua itakuwa kama fainali, nawaamini wachezaji wangu na tutafanya vizuri na kuibuka washindi," alisema Gomes
Mchezo dhidi ya Yanga utapigwa Julai 03 uwanja wa Benjamin Mkapa
Kabla ya mchezo huo, Simba inakabiliwa na mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Azam Fc, mchezo utakaopigwa Jumamosi, Juni 26 2021