Baada ya klabu ya Yanga kuachana na wachezaji waliokuwa Manahodha, Papy Tshishimbi na Juma Abdul, winga kiraka Deus Kaseke amepewa majukumu ya unahodha wakati huu Yanga ikianza maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom
Ukimuondoa Said Juma Makapu, Kaseke na Haruna Niyonzima ni wachezaji waliodumu kwa muda mrefu zaidi kwenye kikosi cha Yanga licha ya kuwa waliondoka na kurejea
Makapu yeye alijiunga na Yanga mwaka 2014 na hakuwahi kuondoka, kwa sasa ndiye mchezaji 'legendary' zaidi kwenye kikosi cha Yanga baada ya Kelvin Yondani na Juma Abdul kuachwa
Kaseke ni mchezaji mwenye nidhamu, mpambanaji na anapokuwa dimbani, hujitoa sana kwa ajili ya timu
Alimaliza msimu uliopita na kiwango kizuri, kama kiongozi, kila mmoja anategemea mambo mazuri zaidi kutoka kwake msimu ujao unaoanza Septemba 06