Leo majira ya saa moja usiku, mabingwa wa nchi Simba watakuwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa kupepetana na Mbeya City ukiwa ni mchezo wa ligi kuu
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amethibitisha kuwa nyota wawili wa kikosi cha kwanza Aishi Manula na Taddeo Lwanga watakosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Lwanga na Manula walionyeshwa kadi za njano katika mchezo uliopita dhidi ya Polisi Tanzania, mchezo ambao Simba ilishinda bao 1-0 mkoani Mwanza

Aidha nyota mwingine atakayekosekana ni kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu ambaye ni mgonjwa
Simba inahitaji kushinda mchezo huo ili kusogea karibu zaidi ya ubingwa nne mfululizo
ADVERTISE HERE