Gomes ataka kukamilisha hesabu za ubingwa mapema

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Jun 2021
Gomes ataka kukamilisha hesabu za ubingwa mapema

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa CCm Kirumba

Akizungumza katika mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Nyamagana jana, Gomes alisema wana malengo ya kushinda ubingwa mapema hivyo wanahitaji kushinda mchezo dhidi ya Polisi

"Tumeweka malengo, tunahitaji kushinda ili tuweze kuwa mabingwa. wachezaji wote wana morali ya juu kuelekea mchezo dhidi ya Polisi Tanzania"

"Tumekuwa na changamoto kadhaa kwenye kujilinda katika michezo iliyopita, tumefanyia kazi hilo. Pamoja na kuwa sisi tuna timu bora lakini ni muhimu kujikumbusha baadhi ya majukumu. Mara nyingi nimesema, nina wachezaji wazuri na najivunia kuwa kocha wao," alisema Gomes

Kimahesabu, Simba inahitaji kushinda michezo mitatu tu ili kuibuka na ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo

Ushindi dhidi ya Polisi Tanzania utawasogeza mabingwa wa nchi karibu zaidi na ubingwa

Inawezekana kabisa, mchezo dhidi ya Yanga Julai 03 Simba ikaingia uwanjani ikiwa tayari ni bingwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
9h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
9h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
12h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’